Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth Mayanja amemvua madaraka
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunda B, Bw. Laurent Agustino kwa
tuhuma za kushiriki kusaidia mwanafunzi mmoja kufanya udanganyifu
katika mtihani wa darasa la nne.
Mwalimu
huyo anatuhumiwa kumruhusu mwanafunzi wa darasa la tano kufanyia
mtihani wa mwanafunzi wa darasa nne kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi
huyo ambaye hajui kusoma wala kuandika ili aweze kufaulu.
Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Kufuatia
tukio hilo Bi. Janeth ametoa onyo kwa walimu wote wa shule zilizofanya
vibaya na kuwataka kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani kwa mwaka
2017 na kuahidi kuwavua madaraka walimu wa shule zitakazofanya vibaya.
Aidha,
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amewataka walimu
wakuu, waratibu na walimu wote kutekeleza kutekeleza majukumu yao
kulingana na sheria na kanun9 a utumishi wa Umma.
Mkurugenzi
huyo amezizawadia shule kumi za Msingi zilizofanya vizuri katika
mtihani wa kumaliza Darasa la saba kwa mwaka 2016 kwa ajili ya kuboresha
kiwango cha elimu katika eneo hilo.
Utaratibu
huo ulenga kutoa hamasa kwa wanafunzi na walimu wilayani humo na
kuongeza juhudi katika kufundisha na kujifunza kwa ajili ya kuongeza
kiwango cha ufaulu katika Halmashauri hiyo.
Amezitaja
shule zilizoingia kumi bora ni pamoja na Olympus, Daystar, St. Paul,
Mzuma, Kabarimu B, Bigutu, Bukore, Kung’ombe, Kabarimu A na Bitaraguru
ambazo zote zimetunukiwa vyeti vya kutambua mchango na juhudi
wanazofanya.
Mayanja
alisema kuwa kati ya shule hizo nne ni shule binafsi na sita za
Serikali ambazo ambapo pamoja na zimekabidhiwa hundi za fedha.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment