MAHALI MKOA ULIPO: Mkoa
wa Mara una eneo la ukubwa wa Kilomita za Mraba zipatazo 30,150. Kati
ya eneo hilo Kilomita za mraba 10,942 ni eneo la maji sawa na asilimia
36 na Kilomita za mraba 19,208 sawa na asilimia 64 ni eneo la Nchi kavu.
Katika eneo la Nchi kavu, Kilomita za mraba 7,258 ziko katika Hifadhi
za wanyamapori, ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mapori ya Akiba ya
Ikorongo na Grumeti na Hifadhi za Jamii Grumeti na Ikorongo. Ukiondoa
eneo hilo Mkoa hubakia na Kilomita za mraba 11,950 kwa ajili ya kilimo,
mifugo na makazi. Mkoa unapakana na Nchi ya Kenya kwa upande wa
Kaskazini, Mkoa wa Kagera upande wa Magharibi, Mikoa ya Mwanza na Simiyu
kwa upande wa Kusini na Mkoa wa Arusha kwa upande wa Mashariki.
Mkoa una jumla ya wakazi 1,743,830 kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012. Kwa ongezeko la asilimia 2.5 kwa mwaka. Mkoa unakadiriwa kuwa na watu wapatao 1, 940,778 kwa mwaka 2016 na utakuwa na idadi ya watu 1, 989,134
ifikapo Desemba 31, 2017. Mtawanyiko wa watu ni watu 61 kwa kila
kilomita moja ya eneo. Jina la Mkoa wa Mara limetokana na Mto Mkuu wa
Mara ambao umeanzia maeneo ya nchi jirani ya Kenya na kutiririsha maji
yake kwa kupitia Wilaya za Serengeti, Tarime, Musoma Vijijini hadi Ziwa
Victoria. Mkoa upo kwenye latitudes 10 0’ na 20 31’, Kusini mwa Ikweta
na katikati ya longitudes 330 10’ na 350 15’, Mashariki mwa Griniwichi
Mkoa wa Mara, ni Mkoa
uliotoa mwasisi wa kwanza wa Taifa ambaye ni Hayati Mwl.Julius
K.Nyerere. Mwalimu alizaliwa Kijiji cha Mwitongo Wilaya ya Butiama Mkoa
wa Mara. Mwasisi huyu wa Taifa aliongoza Tanzania kwa muda wa miaka 23
tangu mwaka 1962 hadi 1985 alipoamua kuachia madaraka kwa hiari yake
mwenyewe. Mwalimu alizaliwa mwaka 1922 na alifariki mwaka 1999. Vilevile
Mkoa wa Mara una mbuga kubwa ya wanyama duniani inayoitwa Serengeti.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya maajabu ya dunia kutokana na
Ukubwa wake na wingi wa wanyamapori wanaopatikana hifadhini.
UTAWALA:Mkoa
umegawanyika katika wilaya sita (6) za Musoma, Butiama, Bunda,
Serengeti, Tarime na Rorya na Halmashauri kumi (9) ambazo ni Bunda (W),
Butiama , Musoma (W), Musoma Manispaa, Rorya (W),Bunda Mji, Serengeti
(W), Tarime (W), Tarime Mji, Mugumu-Mji mdogo
CHANZO TOVUTI YA MKOA WA MARA
0 comments:
Post a Comment