Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Kisorya, wilaya ya Bunda alipokutana nao baada
ya kukagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51
inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Mara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika ziara ya ukaguzi
wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51
inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi
Lugola, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, akiteta jambo na
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati
wa ukaguzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51
inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano
wa sehemu ya barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51
inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano
wa sehemu ya barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50
inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia
54. Barabara hiyo inajengwa na wakandarasi wazawa M/S Mbutu JV.
…………………
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka
mkandarasi Nyanza Road Works kukamilisha ujenzi wa barabara ya
Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi
Novemba mwaka huu.
Prof.
Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo na
kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya na kusema kuwa usanifu wa
barabara na madaraja katika barabara hiyo umewasilishwa sasa ni jukumu
la mkandarasi kuendelea na ujenzi kwa kasi na kwa viwango vya ubora.
“Serikali
ina nia njema kwa wananchi wa wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara sasa
tunaijenga barabara hii na mwishon mwa mwaka mtaanza kunufaika nayo”,
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa kukamilika kwa barabara hiyo utarahisisha mawasiliano na kupunguza
gharama za shughuli za usafirishaji wa samaki, mazao na abiria,
uboreshaji makazi na kukuza uchumi kwa maeneo yaliyo kando ya barabara.
Kuhusu
suala la fidia, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa Serikali italipa fidia
kwa mwananchi ambaye barabara imemfuata kama anavyostahili.
“Serikali
haina nia ya kumuonea mtu yeyote bali inachofanya inalipa kulingana na
sheria inavyoelekeza”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya
Makutano-Sanzale KM 50 na kumwagiza mkandarasi wa M/S Mbutu JV
Contractor (T) kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kabla ya mwezi Julai
mwaka huu.
“Mradi
huu ni wa muda mrefu sana na wananchi wameusubiri kwa muda kama
hamtamaliza mradi huu mpaka mwezi juni, hii itakuwa kazi yenu ya mwisho,
maana ninategemea nyinyi kama wazawa mngekuwa wa mfano” amesisitiza
Prof. Mbarawa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema kwa sasa mkoa
umeamua kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa miradi ya barabara kila
baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mara, Mhandisi Mlima
Ngaile amesema Wakala utasimamia mradi wa ujenzi wa barabara hizo na
kuhakikisha mradi unazingatia viwango kulingana na mkataba.
Waziri
Prof. Mbarawa yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili akiwa na lengo
la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya Ujenzi,Uchukuzi
na Mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment