Makamu wa Rais, Dr. Mohamed Gharib Billal (kulia) na Balozi wa Korea,Mh. Young Kim wakikata utepe kuzindua Chuo cha Ufundi Veta,Mkoani Manyara kikiwa ni Chuo pekee kilichopo mkoani Manyara. Mkoa huo ni moja ya mikoa mipya ambao hauna chuo kingine chochote cha elimu yoyote zaidi ya hiki chuo cha Veta kilichozinduliwa leo.Uzinduzi huo, uliofanyikia katika mji wa Babati, umefanywa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Mohamed Gharib Bilal aliyeandamana na Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Philip Mulugo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Eng. Zebadiah Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi akimuonyesha Makamu Rais, baadhi ya zana za kilimo zitakazotumiwa na Chuo kipya cha Veta Mkoani Manyara.
0 comments:
Post a Comment