Home » » RC MARA AFUNGUA SEMINA KUHUSU SENSA MKOANI MARA, AAGIZA KUKAMATWA WATAKAOLIKWAMISHA ZOEZI HILO.

RC MARA AFUNGUA SEMINA KUHUSU SENSA MKOANI MARA, AAGIZA KUKAMATWA WATAKAOLIKWAMISHA ZOEZI HILO.


 Mmiliki wa blog ya MWANA WA AFRIKA Augustine Mgendi akiwa na mwakilishi wa blog ya Mara yetu Shomary Bonda.


 Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya ya mkoa huo na viongozi wengien wa Serikali. (Picha zote na Augustine Mgendi)


SERIKALI mkoani Mara, imeviagiza vyombo vya dola na viongozi mbalimbali wa ngazi zote mkoani humo, kuhakikisha wanasimamia hali ya usalama kwa kuwachukulia hatua kali watu wote ambao wataonekana kukwamisha mafanikio ya zoezi la Sensa ya watu na makazi,ambalo linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa mjini Musoma na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabiriel Tupa wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya wakufunzi wa Sensa ya watu na makazi ngazi ya mkoa.

Alisema serikali haitakubali baadhi ya watu kuwa chanzo cha kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa taifa na ambalo linatarajia kiasi kikubwa cha fedha,ambapo amesema ni wajibu wa kila kiongozi kufanya uhamasishaji kwaajili ya kuwezesha mafanikio katika zoezi hilo.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alitumia nafasi hiyo kuonya kwamba kamwe serikali hatasita kuchukua hatua kwa wakufunzi hao na kwamba haitakubali kupokea visingizio vya aina yoyote kutoka kwao baada ya kupata mafunzo hayo.

Kuhusu wasiwasi wa wananchi wa kupoteza muda wakati wa zoezi hilo,mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alisema zoezi la sense halitaweza kukwamisha shughuli za wananchi kiuchumi na kwamba watoe taarifa sahihi kwa makarani bila ya hofu  kwa vile taarifa hizo mbali na kuwa za siri pia zitawezesha taifa kupanga mipango yake mbalimbali ya maendeleo

Chanzo: MWANA WA AFRIKA BLOG.




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa