Mara
WATU watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika kijiji cha Kusenye Kata ya Suguti katika halmashauri ya Musoma vijijini mkoani Mara
Afisa Mtendaji wa kata ya Suguti Bw Jackson Marwa akiongea kwa njia ya simu kuwa ajali hiyo imetokea juzi majira ya jioni.
Amesema ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na gari yenye namba za usajili T 752 BQR iliyokuwa ikiendeshwa na Bw Anthony Kusaga wakati akitokea Manispaa ya Musoma kwenda katika kijiji cha Saragana.
Amesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi na hivyo kushindwa kuimudu wakati alipokuwa katika kona karibu na ya zahanati ya kijiji hicho.
Hata hivyo afisa mtendaji huyo amewaja watu waliokufa katika ajali hiyo ni Regina Mwelo mwenye umri wa mika 5,Nyakwesi Mwelo mwenye umri wa miaka 15 na Asha Mwelo mwenye umri wa miaka 17.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Kamisha msaidizi Mwandamizi Abslom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa gari hilo
Hababari kwa hisani ya MWANA WA AFRIKA BLOG
Hababari kwa hisani ya MWANA WA AFRIKA BLOG
0 comments:
Post a Comment