na Igenga Mtatiro, Tarime
BIDHAA zilizopitwa na muda, zisizokidhi viwango na zile zenye viambata vya sumu zimeteketezwa kwa moto wilayani Tarime na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Zoezi hilo liliendeshwa jana pia na Mamlaka ya Chakula na Dawa mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya, Patrick Makinda, chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi na maofisa wa mazingira, nje kidogo ya mji mdogo wa Sirari.
Tanzania Daima lilishuhudia bidhaa hizo zikiteketezwa kwa moto katika eneo maalum lililotengwa ikiwa ni mara ya pili kwa bidhaa za aina kuteketezwa.
Bidhaa zilizoteketezwa kwa mujibu wa Ofisa Udhibiti Ubora, Kituo cha Sirari, Stephen Rwabunywenge, ni kopo 192 za maziwa ya watoto aina ya Cerelac yaliyokutwa yakiwa yamepitwa muda wake wa matumizi na vipodozi aina ya Tenta Claire Carolight ambazo zina viambata vya sumu aina ya Hydroquinone.
Rwabunywenge alisema bidhaa kutoka Uganda na nchi zingine za Ulaya zilikamatwa zilipokuwa zikilipiwa ushuru ambapo uhakiki wake ulibainika kuwa zilikuwa hazikukidhi viwango vya ubora.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment