na Sitta Tumma, Tarime
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana (Bavicha) Taifa la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Tarime mkoani Mara, mwaka 2015.
Heche alisema kuwa, iwapo dhamira yake hiyo itapewa baraka na chama chake, kwa kupitisha jina lake, atahakikisha anapigania maendeleo makubwa ya wananchi wa Tarime, ikiwa ni pamoja na kuwanusuru na umasikini uliokithiri.
Kada huyo aliyasema hayo juzi wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika viwanja vya sokoni, Sirari, ambapo pamoja na mambo mengine, aliirushia kombora Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa imehindwa kutumia vizuri rasilimali za nchi kuleta maendeleo.
Alisema, msukumo wa kutaka kugombea ubunge unatokana na uchungu alio nao wa kutaka kuweka chemichemi kubwa ya mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo, pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha wakazi wa Tarime na Watanzania wote.
"Huu ni wakati wa ukombozi wa nchi hii. Maana Serikali hii ya CCM imeshindwa kabisa kuwasaidia wananchi wake!. Rasilimali za kila aina, zipo hapa Tanzania, lakini zinawanufaisha watu wa nje ya nchi.
"Kwa maana hiyo, mwaka 2015 kama Mungu ataniweka hai nitagombea ubunge Tarime. Kama chama changu kitanipitisha, nimejipanga vizuri kuhakikisha ninaleta mabadiliko ya kimaendeleo hapa," alisema Heche.
Kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali za taifa, mwenyekiti huyo alimshutumu Rais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa kujenga uchumi wa ndani ya nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo, badala yake rasilimali hizo zinayanufaisha wageni.
Alisema, licha ya kuwepo kwa madini ya almasi, dhahabu, makaa ya mawe, nyuklia, gesi na madini yanayotengeneza ndege na kompyuta, maziwa, bahari, mbuga za wanyama na milima mikubwa, watanznaia wanazidi kuteseka kwa umasikini wa kutupwa.
"Tanzania ina kila aina ya madini, lakini umasikini ndiyo unazidi kuota mizizi na kuwatesa Watanzania. CHADEMA hatukubaliani na hali hii, tujiandaeni tuiondoe CCM kupitia sanduku la kura mwaka 2015," alisema Heche.

Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment