Home » » MARA WATAHADHARISHWA NA UGONJWA WA EBOLA

MARA WATAHADHARISHWA NA UGONJWA WA EBOLA

Mwandishi wetu, Mara

Wananchi Mkoani Mara wamepewa tahadhari juu ya Ugonjwa wa Ebola kufuatia kuibuka kwa ugonjwa huo nchini Uganda.

Mratibu wa Elimu ya Afya na Malaria Mkoani Mara Tukae Lisso,amesema maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni kanda ya magharibi ya nchi hiyo ya Uganda ambapo mpaka jana takriban watu 36 wamepata maambukizo na kati ya hao 19 wamepoteza maisha.

Amesema kutokana na taarifa hizo kutoka nchi jirani Wizara ya Afya na ustawi wa jamii nchini imetoa tahadhari kwa wananchi waliopo mikoa inayopakana na nchi jirani ya Uganda kuwa makini na ugonjwa huo.

Tukae Lisso ametaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na mkoa wa Mara,Mwanza,Kagera,Kigoma na Rukwa ambapo wananchi katika mikoa hiyo wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa kutokana na ugonjwa huu wa Ebola.

Amesema dalili za ugonjwa wa Ebola ni pamoja na homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, Kuumwa kichwa na vidonda kooni.

Lisso alisema kuwa wakati mwingine dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi huku figo na ini hushindwa kufanywa kazi.

Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa