Na George Ramadhan
Jamii ya wavuvi katika Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara, imesema kwamba mfumo unaotumiwa na serikali hivi sasa kukabili uvuvi haramu wa sumu umeshindwa.
Badala yake, jamii hiyo imeshauri kutumika mbinu zilizotumika wakati wa utawala wa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza wakati wa maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi katika Kata ya Kisorya (VFA), Msimu Mganga, alisema uvuvi haramu wa sumu unazidi kushamiri licha ya madai ya serikali kuwa inakabiliana nao kikamilifu.
Alisema mfumo wa sasa unaonekana kuchochea zaidi uvuvi haramu kutokana na viongozi hususani wa vijiji, kata na wilaya kuwakamata wahalifu na kisha kuwaachia pasipo kuwafikisha mahakamani.
Alifafanua kuwa hata pale ambapo raia wema wanajitolea kutoa taarifa za watu wanaofanya uvuvi haramu wa kutumia sumu, taarifa hizo huvuja na kuwafikia wahalifu na hivyo kuhatarisha maisha yao.
Aliongeza kwamba siku hizi watu wanafanya uhalifu wa wazi lakini wanaendelea kutamba mitaani, hali inayowakatisha tamaa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za siri.
Aliishauri serikali kuanza kuchunguza magari ya kubebea samaki ambayo yanapofika maeneo ya uvuvi hujaa samaki katika kipindi kifupi hali inayoonyesha kuwepo kwa uvuvi haramu wa kutumia sumu ambao huua samaki wengi.
Akizungumzia athari zinazotokana na uvuvi haramu wa kutumia sumu, Mganga alisema unasababisha samaki kuhamia katika maji marefu hali ambayo husababisha wavuvi wasio na mitaji mikubwa kushindwa kumudu shughuli za uvuvi.

Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment