Home » » MGOMO WA WALIMU MARA KUENDELEA HADI KIELEWEKE

MGOMO WA WALIMU MARA KUENDELEA HADI KIELEWEKE


·       Tarime wanafunzi waandamana kudai haki ya masomo

Shomari Binda, Mara

CHAMA cha walimu Mkoa wa Mara (CWT) kimesema kitaendelea na mgomo ulioanza jana bila kikomo hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai ya walimu hao licha ya wanafunzi wakiingia mtaani kwa maandamano kudai haki ya masomo.

Msimamo huo ulitolewa na Katibu wa Chama cha walimu Mkoa wa Mara Fatuma Bakari, na kusema kuwa hawatishiki na vitisho vya serikali juu yao.

Alisema haiwezekani walimu kuendelea kunyanyaswa kimaslahi na kuonekana kazi wanayoifanya si lolote katika jamii huku wakiishi maisha ya dhiki  wakati Serikali ikiendelea kulikalia kimya suala hilo.
Katika hali isiyo ya kawaida Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi Wilayani Tarime wameandamana hadi ofidi ya Ofisa Elimu wa Wilaya hiyo, wakidai haki zao za kupata elimu baada ya walimu wao kugoma kuingia madarasani na kisha kuwataka wanafunzi kuondoka kwenda majumbani kwao .
Wanafunzi hao walisikika wakiimba na kuongea  mbele ya Ofisa Elimu wa Wilaya Emanuel Jonson. “Watoto tunataka haki zetu, Watoto tunataka  kupata elimu,  watoto tunataka kusoma tunaomba walimu walipwe madai yao tuingie madarasani, watoto tusinyimwe haki yetu ya kupata elimu walimu wanapogoma waathirika ni sisi wanafunzi Serikali tatueni mgomo wa walimu”.
Ofisa Elimu Johnsoni aliwatuliza watoto hao na kuahidi kutatua tatizo la walimu wao na hivyo kuwataka kurejea shuleni siku ya kesho ili kuendelea na masomo kama kawaida.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa