Na Mwandishi wetu, Bunda-Mara Yetu
MWANDISHI wa habari Cyprian Musiba Nyamagambile (34), amechukuwa fomu ya kugombea, nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM), kutoka wilaya ya Bunda na kuahidi kwamba iwapo akipata nafasi ya u-NEC, ataunda hoja ya kuboresha masilahi ya mabalozi wa nyumba kumi.
Musiba ambaye pia ni mkurugenzi wa Gazeti la Afrika Leo, linalotoka kwa wiki mara moja, amechukuwa fomu hiyo ya NEC katika ofisi ya CCM ya wilaya ya Bunda na kukabidhiwa na mkurugenzi msaidizi wa uchaguzi wa wilaya ya Bunda, ambaye pia ni katibu msaidizi wa CCM, na mhasibu wa chama hicho wilayani hapa, Sosteness Mitti.
Wakati akichukuwa fomu Musiba ambaye pia mwaka 2010 aligombea ubunge wa jimbo la Mwibara lakini akashindwa kwenye kura za maoni, amesindikizwa na kundi kubwa la waandishi habari wa mkoani Mara, wanaoandikia vyombo mbalimbali vya habari, waliokuwa na msafara wa zaidi ya pikipiki 20.
Mitti akimkabidhi fomu hiyo amesema kuwa Musiba amekuwa mwanachama wa 14 kuchukuwa fomu hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari Musiba amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo kutokea wilayani Bunda, kwa sababu ni haki yake ya msingi kama mwananchama wa CCM.
Amesema Kuwa iwapo akichaguliwa kuwa mjumbe wa NEC, atajitahidi kujenga hoja ya kuboresha hari za mabalozi wa nyumba kumi, ili waweze kujengewa uwezo wa kimaslahi na kuongeza kuwa siasa ya sasa inazo changamoto nyingi ambazo yeye atazijengea hoja kwenye NEC.
Aaidha, amesema pia katika vikao vya NEC atakuwa anawakisha kero mbalimbali za wananchi bila hoga wala kuteteleka ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kuzitatua.
Katika hatua nyingine Bw. Musiba ameiomba taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) kuanza kazi ya kufuatilia wagombeaji wa nafasi mbalimbali za uongozi, ili chaguzi hizo zisitawaliwe na vitendo vya rushwa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment