Home » » MWANAMKE AUAWA KWA TUHUMA ZA UCHAWI

MWANAMKE AUAWA KWA TUHUMA ZA UCHAWI

Na Shomari Binda, Musoma
MKAZI wa Kata ya Nyakato, Manispaa ya Musoma, Bibi Majira, ameuawa na wananchi wenye hasira, baada ya kutuhumiwa kushiriki vitendo vya kishirikina.

Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, alisema mwanamke huyo alifariki dunia baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara, kutokana na kupata jeraha kubwa la panga katika upande wa kushoto wa kichwa chake.

Alisema si vyema kujichukulia sheria mikononi na kupoteza uhai wa mtu kwa imani za kishirikina na kitendo hicho ni kinyume cha haki za binadamu.

Alisema wataendelea kufanya uchunguzi na mwananchi yeyote atakayebainika kuhusika katika tukio hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Awali, wakizungumza katika eneo la tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema wameamua kuchukua sheria mkononi kutokana na kudai kuwapo kwa matukio ya kishirikina katika Kata hiyo.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa