Mara
WAKULIMA wa vijiji zaidi ya saba katika kata ya Bisimwa na Buruma katika wilaya mpya ya Butiama wameshindwa kuuza pamba yao hadi sasa baada ya kukosa wanunuzi wa zao hilo.
Wakulima hao ni wa vijiji vya Nyabaikwabi,Bisumwa na Nyamajojo katika kata ya Bisumwa na vingine vya kata ya Buruma katika wilaya hiyo mkoani Mara.
Akizungumza kwa njia ya simu mwenyekiti wa serikali ya kijiji Nyabekwabi Bw Mwita Machogu kwa niabaya wenzake,amesema wananchi wa vijiji hivyo wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa baada ya kushindwa kuuza zao hilo msimu huu.
Amesema tangu wananchi wa vijiji hivyo wavune zao hilo la Pamba hawajapata Mnunuzi na hivyo kupelekea hali yao ya Maisha kuendelea kuwa ngumu siku hadi siku huku wananchi hao wakiwa wametumia fedha nyingi kulima zao hilo.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo serikali ya kijiji cha Nyabaikwabe,amesema kuwa mbali na zao la Pamba lakini pia zao la Mhogo kwasasa limekumbwa na ugonjwa ambapo unasababisha zao hilo kuoza likiwa ardhini.
Amesema hatua hiyo inasababisha debe moja la Zao hilo Muhogo kuuzwa kuazia shilingi elfu saba mpaka elfu nane hivi sasa,huku diwani wa kata ya Bisumwa Bw Magina Magesa akikiri kuwapo kwa hali hiyo ambayo imewaathiri wakulima.
Chanzo: Mwanawaafrika blog
0 comments:
Post a Comment