Home » » Ajali yaua 13, yajeruhi 15

Ajali yaua 13, yajeruhi 15







Watu 13 wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Musoma, mkoani Mara.



Ajali hiyo ilitokea juzi jioni katika kijiji cha Mkiringo nje kidogo ya Manispaa ya Musoma.

Katika ajali hiyo, watu tisa walikufa papo hapo fariki huku wanne  wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.

Miongoni mwa watu walifaki dunia ni pamoja na askari wawili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma huku wengine 15 wakiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Mashuhuda wa ajali hiyo na baadhi ya abiria walikuwa katika gari hilo dogo aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 123 CAE lililokuwa likitokea mjini Musoma kwenda kijiji cha Nyamuswa wilayani Bunda, walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kujaza abiria kupita kiasi na mwendo kasi.

Walisema kuwa mwendo kasi ulisababisha kupasuka gurudumu la nyuma upande wa kulia kisha kupinduka na kuua watu tisa papo.

Julius Masato, shuhuda wa ajali hiyo, alisema aliliona gari hilo likiwa katika mwendo wa kasi likiwa na abiria wengi kabla ya gurudumu kupasuka na kupinduka.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk. Joseph Nyamagwira, alisema kutokana na baadhi ya majeruhi hao kujeruhiwa vibaya  na wengine kuvunjika viungo vyao vya mwili, watalazimika kuhamishiwa haraka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya uhakika.

Dk. Nyamagwira alisema kuwa baadhi marehemu ambao wamehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali hiyo ni pamoja na Esther John na Emmanuel Joseph, ambaye alikuwa dereva wa Hiace hiyo.

Kwa mujibu wa Dk. Nyamagwira, miili mingine inayohifadhiwa katika hospitali ya mkoa ni  ya Pendo James na mtoto wake, Joseph Richard pamoja na Razack Shaban, wakazi wa kijiji cha Nyamuswa.

Wengine ni Hamis Kanyoro Richard, Makuri Magori, wakazi wa Bisarya; Nyamazare John, Innocent Kweka, Richard Said Dogori, Hassan Masoke na mmoja ambaye ametambulika kwa jina moja la Isaac. Wote  hawajafahamika meneo wanayotoka.

Baadhi ya ya majeruhi katika ajali hiyo wametajwa kuwa ni Betty Ngutu, Elfansia Kamanzi, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chief Ihunyo.

Wengine ni Busegwe, Mather Makori na wengine ambao hali zao ni mbaya hawajafahamika. 

Pia wamo Hamis Isaac na Beatrice Sirima Isaac na Sirima walisema kuwa baada ya kufika katika eneo la Mkiringo gari lao lililokuwa katika mwendo kasi lilijaribu kulikwepa gari lingine na ndipo lilipopasuka gurudumu la nyuma na kuchomoka wakiwa katika mteremko na gari kupinduka mara tatu.

Kuhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, hazikufanikiwa kutokana na simu zake zote za kiganjani kufungwa.

habari NA GEORGE MARATO 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa