Home » » BUNDA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU EPZA

BUNDA YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU EPZA

na Berensi Alikadi, Bunda
KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bunda imesitisha kwa muda malipo ya fidia ya sh bilioni 1.2 kwa wananchi wa Kitongoji cha Kirumi ambao wanatakiwa kupisha eneo hilo kwa shughuli za uwekezaji za EPZA baada ya kubaini kuwapo kwa majina hewa.
Mwenyakiti wa kamati hiyo, Joshua Mirumbe, ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, alisema wakati fedha hizo zinapelekwa kulikuwa na shughuli ya sensa ya watu na makazi na pia wilaya ilikuwa ina maandalizi ya kupokea mwenge wa uhuru, hivyo kamati haikuweza kuhakiki majina ya watu wanaostahili kulipwa.
Alisema wakati kamati hiyo inajipanga, ilishangaa kuona halmashauri ya wilaya imeshaanza kuwalipa wananchi wa kitongoji hicho bila mpangilio, jambo alilosema lingeweza kuleta manung’uniko makubwa kwa wananchi wengine.
“Tumepata taarifa ya kuwepo kwa majina hewa ya watu ambao pia walijiandikisha kuwa wanaishi katika kijiji hicho wakati ni uongo, watu hao wanaishi hapa mjini… atakayebainika kughushi jina atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Mirumbe.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa