Anthony Mayunga, Nyamongo
POLISI Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, wanadaiwa kuwajeruhi kwa mabomu ya machozi watu sita katika operesheni ya kuwatawanya waliovamia kifusi cha mawe kutoka mgodini.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa sita mchana katika Kitongoji cha Nyabikondo, Kijiji cha Kewanja wilayani Tarime.
Tukio hilo limetokea katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja baada ya Polisi kutumia nguvu kutawanya wafuasi wa Chadema mkoani Morogoro na Iringa ambako watu wawili, mmoja katika kila mkoa alifariki dunia. Aliyefariki Morogoro ni Ally Zona na wa Iringa ni Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi. Katika matukio hayo, watu wengine kadhaa walijeruhiwa.
Katika tukio la Tarime, polisi hao wanadaiwa kutumia mabomu hayo kuwatimua wananchi hao hadi majumbani au maeneo yao ya kazi.
Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Suzana Mwita Gibaye (28) ambaye aliumia kichwani na mguu wa kushoto na Ghati Marwa ambaye ni mjamzito na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Wengine ni Esther Chacha (12) Chacha Chacha (10) na Daniel Chacha(6) pamoja na mama yao Magaiwa. Hao wanadaiwa kujeruhiwa kwa mabomu hayo wakiwa nyumbani kwao wakiendesha biashara ya mgahawa.
Akizungumzia tukio hilo, Suzana alisema alijeruhiwa na mabomu hayo muda mfupi baada ya kutoka katika Zahanati ya Kampuni ya African Barrick North Mara kutibiwa.
“Tukiwa tunaendelea na kazi kwenye eneo la Mrwambe, tuliona polisi wanafukuzana na vijana waliovamia kifusi kilichomwagwa nje ya mgodi huku wakipiga mabomu. La kwanza na la pili hayakutufikia, walipopiga bomu la tatu nikashtukia napigwa kichwani na kitu, mguu wa kushoto damu zikaanza kuvuja nikaanguka.
“Lilifika gari la pili la polisi, ofisa mmoja akawachukua watoto na mama yao, mimi nilikuwa nimeanguka kwa chini, hawakuniona. Wakawapeleka zahanati ya mgodi, mimi nilichukuliwa na bodaboda hadi Hospitali ya Sungusungu wakaniambia niwape PF 3, kurudi polisi wakanipeleka zahanati ya mgodi,” alisema.
Mama huyo alifungwa bandeji kichwani na mguuni kisha akapewa dawa na kurudishwa polisi na kutoa maelezo na kisha kuachiwa huru.
Katika vurugu hizo, mashuhuda walisema wananchi nao waliyashambulia magari ya polisi kwa mawe... “Wakati polisi wakirusha mabomu, watu walikuwa wanajibu kwa kurushia mawe gari la polisi,” alisema mmoja wa majeruhi hao.
Viongozi wasimulia
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyabikondo, Charles Vicent alisema tukio hilo lilitokea wakati wakiwa kwenye kikao cha usuluhishi kati ya koo ya Nyabasi na Wanyamongo kilichomhusisha pia Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tarime, wazee wa mila na viongozi wa maeneo husika.
“Tukiwa kwenye kikao mpakani mwa Kewanja na Nyakunguru, ndipo pakatokea matukio hayo ambayo yalimlazimu OCD kukimbilia eneo la tukio na kuwachukua wale watoto na mama yao na kuwapeleka mgodini wakafungwa bendeji. Inasemekana gololi ziliwaumiza kichwani na vifuani,” alisema.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa vurugu hizo lakini akasema kuwa hana taarifa za watu kujeruhiwa kwa mabomu.
“Vurugu ni kila siku tena leo wamepiga sana gari letu kwa mawe. Hapajatokea utulivu eneo hili, maana watu wanajitokeza kwa wingi kutufanyia vurugu. Hapa lazima uamuzi mgumu uchukuliwe ama kuondoa wananchi karibu na mgodi au kampuni iondoke ili watu wachimbe madini kama zamani, maana mgodi uko kwenye makazi ya watu ni hatari sana,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment