Wachache wanaweza kubeba viti kutoka Majumbani kwao
Kwastahili hii kweli tutafika?
Sijiu kama Mwandiko hapa utakuwa mzuri
Naweza kusema huyu ndyo Mtemi Class
Wanafunzi wakiwa darasani makini katika kumsikiliza Mwl huku wakiwa wamekaa chini
Baadhi ya sehemu ya Madawati 1050 yakiwa mbele ya shule za Nyangoto na Matare wilayani Tarime tayari kukabidhiwa kutoka mgodi wa ABG North Mara
Mmoja wa Wanafunzi akifurahia Madawati waliyopewa na Mgodi wa ABG North Mara
Mbali na Msaada wa Madaftari na vifaa vya shule kwa baadhi ya wanafunzi wa sekondary Pia Mgodi huo ulitoa Bajaji kwa watu watatu wasiojiweza
Picha ya Pamoja wanafunzi wa Nyangoto na Matare shule ya Msingi
TARIME
SERIKALI imesema kuwa kamwe haiwezi kumtegemea mwekezaji kwa kila kitu huku baadhi ya Mambo yanaweza kufanywa na wanajamiii wenyewe katika sehemu huska.
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw John Henjewele katika hafla ya kukabidhi Madawati kwa baadhi ya shule zinazozunguka mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) North Mara, Vifaa vya Shule kwa baadhi ya wanafunzi na baiskel ya Magurudumu matatu kwa watu watatu wasiojiweza.
Alisema kuwa pamoja na Misaada inayotolewa na Mgodi huo kwa Jamii lakini pia serikali inashukuru Mahusiano Mazuri yaliyopo katika Mgodi huo wa African Barrick Gold (ABG ) North Mara na Jamii.
Mkuu wa Wilaya huyo aliushukuru Mgodi huo kwa kugundua hali ya Walemavu,kutoa vifaa vya Elimu huku akisema hiyo ni hatua moja mbele katika kuisaidia Jamii.
“Kwanza tushukuru sana Mahusiano yaliyopo kati ya Mgodi huu na Jamii lakini pia hatuwezi kumtegemea Mwekezaji kwa kila Jambo lazima sisi wenyewe tujitoe katika kufanikisha baadhi ya Mambo yetu” alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya Meneja mkuu wa Mgodi wa African Barrick Gold (ABG)North Mara Bw Gary Chapman,alisema Mgodi huo ni miongoni mwa Migodi Afrika ambayo imekuwa ikiwekeza katika Jamii hasa katika suala la Elimu,Afya,Maji na Maendeleo katika Jamii.
Alisema Pamoja na kutotimiza mahitaji kwa shule za Sekondary kwa asilimia mia lakini watajitahidi kushirikiana na Jamii jiyo katika kujiletea Maendeleo.
“Mgodi huu ni moja ya Mgodi Afrika ambao unajitolea katika kusaidia Jamii hasa katika Elimu,afya,maji na Masuala la Maendeleo,lakini pamoja na kutotimiza Mahitaji ya Jamii kwa asilimia kubwa bado tutaendelea kushirikia na nao” alisema Bw Gary Chapman
Aidha Uongozi wa Mgodi huo wa African Barrick Gold umetoa Madawati zaidi ya 1000 kwa shule za Nyangoto na Matare zilizopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara huku Miradi yote Mitatu ya Elimu,msaada ya Baiskel na Madawati hayo ikigharimu kiasi cha shilingi milioni 188.
Watu waliopewa Baiskel hizo za Miguu mitatu ni pamoja na Eliza Mwikwabe ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo,Penina Mseti muuza mboga na Nyanya pamoja na Gesongo Chacha ambaye ni fundi wa kuchomelea vyuma.
Taarifa zinasema kuwa Mgodi huo wa African Barrick Gold (ABG) North Mara umetenga zaidi ya shilingi Bilion 20 katika kipindi cha miaka mitatu kusaidia Makundi mbalimbali ya Kijamii yanayozungukwa na Mgodi huo katika kuyaletea Maendeleo
Awali akisema Risala kwa Mgeni Rasmi Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyangoto Bw Ghati Keraryo alisema kuwa shule zote mbili za Nyangoto na Matare zina jumla ya Madawati 202 kati ya 654 ambayo yanahitajika.
Alisema kwa niaba ya Walimu wa shule hizo wanapenda kutoa shukurani kwa Mgodi wa ABG North Mara kwa kutambua Umuhimu wa Changamoto moja wapo zinazokabili shule hizo ikizingatiwa kwamba shule hizo zipo karibu na Mgodi huo.
Mbali na Msaada huo wa Madawati kwa shule hizo,Msoma risala huyo alisema kuwa bado shule hizo zina upungufu wa Viti 46 na meza 18,huku akiuomba Mgodi huo kuendelea kujenga Shule hizo kama Mkataba ulivyoainisha katika ya Kijiji na Mgodi.
0 comments:
Post a Comment