Baadhi
ya wananchi wa Vijiji zaidi ya 10 vinavyopitiwa na barabara ya Balili
Manchimweru wilaya ya Bunda mkoani Mara wameipongeza Serikali kwa
kuipandisha hadhi barabara hiyo kuwa chini ya TANROAD na pia
kuitengeneza kwa kiwango cha Changalawe.
Sauti
za wananchi hao zimesikika mbele ya waandishi wa habari wakati wa
Matengenezo ya barabara hiyo yenye urefu wa km 41 kupitia Kampuni ya
ukandarasi ya Keres Tanzania LTD.
Wamesema kabla ya ujenzi huo barabara hiyo ilikuwa kero hasa nyakati za Mvua lakini kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha mambo mengi katika maisha yao ya kila siku
Kwa upande wake Fundi Mchundo wa barabara hiyo Bw Charles Joseph amesema
mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilling Milion 300 ulitakiwa
kukamilika ndani ya miezi sita lakini kutokana na Mvua zilizokuwa
zikinyesha ulichelewa kukamilika na hivyo kukamilika mwishoni mwa mwezi
julai.
Kutengenezwa
kwa barabara hiyo kunafuatia malalamiko ya Mara kwa Mara ya Wananchi
hao hasa nyakati za Mvua na hivyo kutengezwa kwa kiwango cha Changalawe
ni faraja kwa wakazi wa Vijiji hivyo
Chanzo: Mwanawaafrika
0 comments:
Post a Comment