SHIRIKA la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia hifadhi ya wanyama Serengeti imetoa msaada wa
mabati elfu sita Wilayani Tarime kama sehemu yao ya kutekeleza
miradi ya maendeleo katika Wilaya na vijiji vinazopakana na Hifadhi za Taifa.
Akikabidhi
mabati hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa Mjini
Tarime,Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi amesema kuwa shirika la
Tanapa limetoa mabati Elfu 6,000 yenye thamani ya milioni 124 kwa
ajili ya kusaidia katika maendeleo ya wananchi wa Tarime.
Kijazi amesema kuwa
mabati hayo yatasaidia kuezeka madarasa ya shule,nyumba za walimu na
vituo vya polisi na Zahanati ndani ya Wilaya ya Tarime nakwamba msaada
huo unatokana na ushirikiano na mahusiano mazuri kati ya Tanapa na Wilaya
ya Tarime.
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Mara John Tuppa amezitaka Wilaya zingine kuwa wabunifu kama
Tarime kwa kuomba wadau mbalimbali ili wawasaidie katika shughuli za
kimaendeleo ambapo pia amewapongeza Tanapa kwa msaada waliotoa kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment