Home » » Machimbo ya kokoto yaua wawili wa familia moja, mmoja ajeruhiwa

Machimbo ya kokoto yaua wawili wa familia moja, mmoja ajeruhiwa

WATU wawili wakazi wa kitongoji cha Kanisani kijiji cha Matare Mamlaka ya mji wa Mugumu wilaya ya  Serengeti Mkoani Mara  wamekufa na mmoja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.

Polisi,uongozi wa Kitongoji na Hospitali Teule ya Nyerere ddh
wamethibitisha kutokea kwa Tukio hilo  limetokea julai 14 majira ya saa 4:10 asubuhi mwaka huu katika eneo la machimbo ya kokoto wakati wakiwa wanachimba.

Mganga wa zamu Dk,Amosi Kittoh amewataja wanawake hao waliofariki na kujeruhiwa kuwa ni Rhobi Mwita Nyantori (39) aliyefia eneo la Tukio, Nyahiri Chacha Mwita(41)amefia hospitali na Majeruhi ni Wegesa Mwita (39)ambaye anaendelea na matibabu.

Dk  Kittoh amesema kuwa tukio hilo limesababisha ndugu wa marehemu hao Joseph Wambura kupoteza fahamu na wamemlaza wodi ya wanaume kwa ajili ya matibabu.

Wegesa ambaye ni majeruhi amesema akiwa ndani ya shimo pembeni na wenzake waliokuwa ndani akisubiri kokoto atoe nje ,ghafla kifusi hicho kikawafunika ,na kuokolewa na wananchi ,baada ya waliokuwa nje kupiga yowe.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Juma Mahando amesema machimbo hayo yalikuwa yamefungwa toka novemba 2009 baada ya watu wawili kuangukiwa na kifusi na kufariki papo hapo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa