HALMASHAURI ya Wilaya
ya Tarime Mkoani Mara imepata hati safi inayolizisha ambapo taarifa ya
fedha imezingatia viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa hesabu za Serikali
(ISA) pamoja na taratibu zingine za kiukaguzi.
Akisoma ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu taarifa ya fedha
za Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa mwaka unaoishia tarehe 30,juni/2012
mbele ya baraza la Madiwani Mkaguzi wa Mkoa wa Mara Mustafa Mwangaile,
alisema kuwa taarifa za fedha zimeakisi kiasi cha kuridhisha mambo yote
yaliyohusika.
Mwangaile amesema
kuwa hali ya fedha ya Halmashauri hadi tarehe 30 juni 2012 na matokeo ya
utendaji wa mapato halisi kwa mwaka ulioisha,inawiana na viwango vya
kimataifa vya uwaandaaji wa hesabu za fedha kwa secta ya umma
(IPSAS).
Aidha mkaguzi
huyo ameisisitiza halmashauri kutumia fedha za ndani na Ruzuku za
serikali kwa wakati pindi zinapopokelewa kwa madai kuwa kiasi cha
420,484,000 zilihamishiwa kwenye akaunti ya shule mbalimbali kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa,maabara,ofisi za shule na kituo cha afya Nyakunguru zilikuwa
bado hazujatumika hadi kufikia juni 2012.
Hata hivyo Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Athumani Akalama alisema kuwa fedha hizo
kutotumika kwa wakati mwafaka ni kutokana na Serikali kuchelewa
kuleta fedha ambapo fedha zingine wamekuwa wakizipokea mwisho wa mwaka na hivyo
kushindwa kutekeleza miradi kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment