SERIKALI wilayani
Bunda mkoani Mara, imewaonywa viongozi wa kisiasa pamoja na watumishi wote wa
seriakali, ambao wanajihusisha ama kufadhili uvuvi haramu, kwamba wakibainika
hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.
Mkuu wa wilaya ya
Bunda, Bw. Joshua Mirumbe, ametoa onyo hilo jana, wakati akizungumza na Radio
Free Africa, baada ya kuulizwa maswali kwamba ni kwa nini uvuvi haramu katika
wilaya ya Bunda, bado uneshamiri sana.
Akijibu maswali hali
hayo mkuu wa wilaya ya Bunda, amesema kuwa ni kweli pamoja na jitihada zake
za kusimamia zoezi hilo la kukomesha uvuvi haramu, bado uvuvi huo
unaendelea kuwepo wilayani humo.
Bw. Mirumbe amesema
kuwa kuna taarifa kwamba baadhi ya viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma
wanajihusisha na uvuvi haramu.
Kutokana na kuwepo
kwa hali hiyo mkuu wa wilaya ya Bunda, ameonya kuwa iwapo kiongozi au mtumishi
yeyote, akibainika atawajibishwa ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za
kinidhamu na za kisheia.
Amesema kuwa katika
jimbo la Mwibara uvuvi haramu hasa umeshamiri katika kijiji cha Kasahunga,
ambako kunadaiwa kuna kuna mvuvi mmoja haramu ambaye ni sugu, anayetuhumiwa
kuhamasisha wavuvi wengine wa vijiji vya Bunere, Nyansimo, Busambara, Mahyoro,
Kasuguti, Mwiseni, Nambuni, Kisorya, Bwanza na Sunsi.
Wananchi wa maeneo
hayo wamesema kuwa katika vijiji hivyo wavuvi haramu wanatumia zana zisizo takiwa
yakiwemo makokolo na kwamba wanapotakiwa na serikali kusalimisha zana hizo
uleta vipande tu, huku makokolo halisi wakiyaacha.
Wananchi hao wamesema
kuwa uvuvi haramu hauwezi kuisha kwani baadhi ya viongozi wakiwemo wa vikundi
vya ulinzi wa rasilimali za ziwa Victoria (BMU), pamoja na polisi, watendaji wa
vijiji na kata, wamekuwa wakifadhili uvuvi huo kwa kupewa mgao kila wiki.
0 comments:
Post a Comment