MKURUGENZI wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Athuman Akalama amezuia
malipo ya fedha zilizotolewa na Serikali Kutoka Tanesco kwa ajili ya fidia kwa
wananchi walioko katika maeneo yaliyopitiwa na njia ya mradi wa umeme vijijini
unaoanzia Mugabiri mpaka Itiryo baada ya tume aliyoiunda kuchunguza na
kuhakiki maeneo kubaini kasoro kadhaa zikiwamo za majina hewa 281.
Akiongea na waandishi
wa habari Mkurugenzi Akalama amesema kuwa mwezi mei ,2013 Halmashaauri
ilipokea fedha bilioni 1,541,546,526,.43 Kutoka Serikalini zilizotolewa
na Tanesco kwa ajili ya kulipa wananchi nakwamba kutokana na malalamiko ya
baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yaliyopitiwa na umeme kutoonekana katika
orodha ya malipo Mkurugenzi alilazimika kuunda tume ya kuhakiki maeneo kabla ya
malipo .
Akama Amesema kuwa
Tume imebaini kuwa kuna majina hewa 281 kati ya majina 1,102 yaliyokuwa
tayali kwa malipo,pia kuna watu 137 waliofanyiwa uthamini kwenye maeneo yao
ambao wana maeneo lakini majina yao hayako kwenye kitabu cha malipo huku
wananchi wengine 140 ambao wana maeneo na mali zao na wamepitiwa na mtandao wa
umeme lakini hawakufanyiwa uthamini.
Akalama anaongeza
kuwa Tume imebaini kuwa kulikuwa na fomu hewa 132 na jumla ya watu
499 taarifa zao zina kasoro na zinatakiwa kufanyiwa marekebisho na kwamba
watu 430 pekee ndiyo wanatakiwa kulipwa kwakuwa taarifa zao ni nzuri
hazina kasoro jambo ambalo limemladhimu kuzuia malipo ili
kushughulikia malalamiko ya wananchi ili wapate haki zao kwakuwa kitabu
cha malipo kina matatizo na zoezi halikufanyika kwa kufuata maadili akawataka
wananchi kuwa wavumilivu.
0 comments:
Post a Comment