Home » » VIJANA UKEREWE SACCOS YAKAMATA MALI ZA WADENI WAKE

VIJANA UKEREWE SACCOS YAKAMATA MALI ZA WADENI WAKE

MALI  za  wanachama  17  wa chama  cha  kuweka na kukopa  cha  Vijana  Ukerewe  Saccos  zimeanza kukamatwa   ili  kufidia   fedha  walizokopa sh. Mil. 14.6 na wakashindwa  kuzirejesha.
Meneja wa  chama hicho  kilichopo   wilaya ya  Ukerewe, Mwanza  Bw,  Ferdinand  Lukansola  amewambia wahandishi wa  habari  ofisini kwake jana kuwa  mali za wanchama hao zinakamatwa ili kufidia mikopo  waliyokopo na kushindwa kurejesha.
Alisema  kabla ya  chama hicho  kuchukua hatua  hiyo  suala hilo lilifikishwa mahakamani na  hivi karibun mahakama ilitoa amli  malizi    zao zikamatwe ili kufidia  madeni yao.
Alifafanua kuwa  baadhi ya  mali  zao  ikiwemo viwanja viwili, thamani za ndani  na mali nyingine  kama  mifugo  vimekamatwa tangu juzi  na baadae  zitauzwa  ili  kufidia  mikopo  hiyo.
 Ilielezwa   kuwa  wadaiwa  wengine  sugu wapatao  189  wanaodaiwa sh. Mil. 97.8 wamepewa muda na chama  hadi septemba  mwaka huu wawe wamerejesha  mikopo hiyo  vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Katika  hatua nyingine  jeshi la polisi  wilayani humo linaendelea na uchunguzi  wa  tuuma ya  wizi  wa sh. Mil. 38.8  zinazowakabili  watumishi wawili wa chama  hicho cha Vijana  Ukerewe Saccos  ili ikithibitika  wafikishwe mahakani.
Meneja wa  Chama hicho Feldinand  Lukansola   alisema   kesi hiyo itafikishwa mahakani  wakati wowote kuanzia  sasa  baada ya  mmoja wa watuumiwa  hao  aliyekuwa  afisa  mikopo wa chama hicho  Denis  Matundane  kukamatwa  juzi.
Mtuumiwa  mwingine  katika kesi hiyo  ni  aliyekuwa keshia  wa chama hicho  Assa Joseph Makole  na  kwamba    watumishi hao walipatika na tuuma hizo baada ya  kufanyiwa ukaguzi na ikabainika  walitumia udanganyifu  na kujipatia   fedha hizo kinyume na taratibu.
Mwenyekiti  wa bodi ya  Vijana Ukerewe Saccos  Vedastus  Toto  alisema wakati akithibitisha  taarifa hizi kuwa  tatizo hilo limesababisha   chama hicho kishindwe kutoa   huduma nzuri  kwa wanachama wake  kwa muda mrefu sasa.
Alisema  tatizo hilo lililoanza tangu  mwaka  2006  pia limesababisha  chama kishindwe kurejesha  kwa wakati  mikopo ya  tasisi za kifedha  ikiwemo  Benki ya CRDB  na  Self  Project .
Hata hivyo  ametumia fursa hiyo  kuwataka  wanachama  wa chama hicho  watambue kuwa   hali ya uvumilivu  imekwisha  kwa yeyote  anayeshindwa kurejesha mkopo kwa  wakati  na  kuwataka  wadaiwa wote watumie muda waliopewa kurejesha mikopo yao vinginevyo taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa