Home » » MWANAFUNZI AJINYONGA BAADA YA KUNYIMWA MAHINDI YA KUCHOMA.

MWANAFUNZI AJINYONGA BAADA YA KUNYIMWA MAHINDI YA KUCHOMA.



KATIKA  kijiji cha Nyabisaga kata ya Kyore Wilayani Tarime, Richard Charles Waitati (14) mwanafunzi wa darasa ka tano katika shule ya msingi St Jude  ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyagisya amefariki dunia baada ya kujinyonga na kamba  ya katani.

Kamanda  wa Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus kamugisha  amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 6 juni majira ya saa 12 jioni  ambapo chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia ambapo marehemu aligombania  muhindi wa kuchoma na wadogo zake.

Kamugisha anaongeza kuwa baada ya kushindwa kuupata  ndipo alipochukua uamuzi wa kujinyonga nakwamba mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na dactari na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa mazishi.

Wakati huo huo,MKAZI  mmoja  wa kijiji cha Genkuru, Matera Marwa Chacha (25) amekutwa akiwa amekufa  na mwili wake kuokotwa katika Kijiji cha Kewanya –Nyamongo Wialayani Tarime akiwa amepigwa kisogoni na kitu butu na michibuko mgongoni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema kuwa  tukio hilo limetokea juni 6 mwaka huu ambapo chanzo cha tukio hilo ni marehemu kulisha mifugo yake kwenye chamba la Mwita Mabya (83) ambaye ni mkazi wa kijiji cha kewanja na kwamba mtuhumiwa amekamatwa yupo kituo cha polisi Nyamwaga.

Kamugisha  amesema kuwa tukio linguine  limetokea katika kijiji cha Gebaso kata ya Nyarukoba Wilayani Tarime   ambapo mkazi wa Gibaso Mkwaya Mwita (48) amejeruhiwa kwa  kukatwa na panga  kiganja  cha mkono wa kulia na kutenganishwa na mkono huo na mtu aitwae Marwa Ngoka ambaye alitoroka  baada ya tukio hilo.

Kamanda kamugisha amesema kuwa  tukio hilo limetoke  6 juni na chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi na kwamba majeruhi amelazwa katika kituo cha afya Masanga na hali yake inaendelea vizuri.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa