Home » » CHUO CHA UTALII CHAPEWA MSAADA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA

CHUO CHA UTALII CHAPEWA MSAADA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA

KAMPUNI ya Singita Grumeti Reserves iliyoko kijiji cha Makundusi kata ya Natta wilaya ya Serengeti Mkoani Mara imetoa msaada wa vifaa vya kufundishia kwa Chuo cha Utalii Serengeti vyenye thamani ya zaidi ya sh.Mil.7

Akikabidhi msaada huo wa Komputa,mahema,viti,meza,vitabu na Ovena Mkurugenzi wa Utalii wa Kampuni hiyo Jason Trollip amesema sekta ya utalii kwa Tanzania ndio inaanza kushika kasi hivyo wao kama wawekezaji wanafanya kila njia kuhakikisha vijana wengi wanapata elimu bora itakayowasaidia kuingia kwenye soko la ajira.

Amesema Kampuni yao ina miliki hoteli saba hivyo kwa kusaidia chuo hicho wanalenga kupata vijana walioiva vizuri kufanya kazi za utalii,ikiwa ni mkakati wa kukuza ajira na kuinua jamii kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa mkakati wao ni kuhakikisha jamii inayowazunguka inanufaika ,hivyo wanajitahidi kusaidia kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya ,maji,barabara na sasa kuna vijana 16 wanawasomesha shule na vyuo mbalimbali hapa nchini na kampuni imetumia sh.44,800,000.

Mapema Mkurugenzi wa chuo hicho Samweli Peter Marwa akitoa taarifa ya chuo amesema vijana 400 waliopita chuoni hapo wamepata kazi na kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kuwapokea kuanzia mazoezi na hata ajira na kuomba makampuni mengine ya uwekezaji wilayani humo kurudisha faida kwa jamii ,kwa kusaidia vijana kupata ajira.

Naye mjumbe wa bodi  ya chuo Suzana Kiroiga ambaye ni diwani viti maalum CCM akitoa shukrani niaba ya bodi amesema kuwa ,wawekezaji wengine wanatakiwa kubadilisha mitizamo waweze kusaidia fursa kama hizo zinazosaidia vijana hasa wasichana kupata elimu badala ya kuingia kwenye ndoa za mapema.




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa