Home » » Kinana, Nape wazuru kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere

Kinana, Nape wazuru kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere


IMG_7745
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiwa katika picha ya pamoja na Andrew Nyerere Mtoto wa Kwanza wa Baba wa taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipozuru kaburi la Mwaasisi huyo wa taifa la Tanzania Mwitongo, Butiama Nyumbani kwa mwalimu Mkoani Mara jana, Kinana alifanyakazi na Andrew Nyerere wakati wakilitumikia Jeshi la Ulinzi la wananchi la Tanzania (JWTZ), Katibu Mkuu huyo jana aliendelea na ziara yake katika wilaya ya Butiama katika kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, Kinana ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Serengeti leo. Kushoto ni Nape Nnayue Katibu wa (NEC) Itikadi Siasa na Uenezi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-BUTIAMA MARA IMG_7746 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Andrew Nyerere mara baada ya kuzuru Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere Mwitongo Butiama jana 4
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiongozwa na ndgu wa Mwalimu Mzee Jack Nyamwaga wakati akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere jana mjini Butiama, Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mama Mabula
721
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati. Mwalimu Julius K. Nyerere huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio hilo. 10Wana habari nao wakishiriki kuweka mashada ya maua katika Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere jana kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangwe Bw. John Bukuku, Said Mwishehe kutoka Jambo Leo Oktavian kutoka CCM Gerson Msigwa wa TBC, Ufo Saro wa ITV na Prosper Dereva wa CCM. 11 
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia akimsikiliza Balozi Safari wakati alipotembelea Shina namba 14 Mwitongo Butiama na kuzungumza na wanachama wa shina hilo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao. 13 
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akisalimiana na Mzee Jack Nyamwaga huku katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kulia akizungumza na mzee Mdogo wa Mwalimu Julius K. Nyerere Daniel Nyerere mara baada ya kumaliza kikao chake na wanachama katika shina namba 14 Mwitongo. 14 
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM kulia akizungumza na Mh. Nimrod Mkono aka “Mkono kwa Mkono”Mbunge wa Jmbo la Musoma Vijijini. 15 
Hili ni Jengo la zahanati ya kata ya Busegwe ambalo ujenzi wake unaendelea kwa kushirikisha Halmashauri ya wilaya ya Butiama vijijini Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mh. Nimrod Mkono na nguvu za wananchi. 16 
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupia lipu wakati alipokagua ujenzi wa zahanati ya Busegwe jana kulia ni Mgendi Sikila mmoja wa mafundi wanaojenga zahanati hiyo. 17 
Katibu Mkuu wa UWT Taifa na Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara Amina Makilagi akishiriki kubeba udongo, wakati Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa zahanati hiyo kata ya Busegwe 18 
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Butiama Dk Wilbert Manase wakati alipotembele ujenzi wa zahanati hiyo. 19Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua ujenzi wa zahanati Busegwe 20Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono akishiriki kucheza ngoma na moja ya vikundi vilivyokuwa vikitumbuiza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 21 

Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuangalia Katibu Mkuu wa UWT Taifa Bi. Amina Makilagi wakati akishiriki kucheza ngoma. 22 
Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mama Mabula akizungumza na wananchi katika kijiji cha Bwai.
23 
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimshukuru Diwani wa kijiji cha Bwai Jamila Nyamanda kupitia TPP Maendelea kwa ushirikiano wake katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM 24 
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo wakati alipokuwa akimsikiliza mzee Nyanda Totela wakati alipokagua Shule ya Msingi ya Bwai Musoma vijijini jana 25 
Shule ya Msingi Bwai inavyoonekana 28 
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM kulia akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kyabakari Butiama jana 29 
Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole na Katibu wa kabila la Zanaki Mzee Peter Nyamrubwe Nyamrubwe kama ishara ya kuwa mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila la wazanaki, kulia ni Mh Nimrod Mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini. 30 

Katibu Mkuu wa CChama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa Gwesani M. Gwesani moja wa makatibu kata waliokabidhiwa baiskeli hizo kwa ajili ya kuimarisha Chama Wilayani Butiama 32 
Baadhi ya ananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa