MSANII wa muziki wa asili Saida
Karoli juzi ameibuka mshindi katika tamasha la ni nani zaidi, kati ya wasanii
wote ambao wamerekodi kazi zao katika studio ya Tivol ya jijini Mwanza.
Tamasha hilo lilifanyika katika
uwanja wa karume mjini Musoma na kuhudhuriwa na wananchi zaidi ya 5,000
kutoka maeneo mbalimbali mkoani humo.
Murugenzi mtendaji wa studio ya
Tivol, Nilivinus Madaraka, jana alisema kuwa katika tamasha hilo, Saida Karoli
aliibuka mshindi, akifuatiwa na Bhudagala Mwanamalonja na nafasi ya tatu
ilishikiliwa na Papaa Kishapu.
Madaraka alisema kuwa tamasha hilo
lilishirikisha wana muziki 16 ambao wote kazi zao zimerekodiwa katika studio
yake na kwamba lengo lake lilikuwa ni kuutangaza muziki wa asili na kuenzi mila
na utamaduni wa mtanzania.
Aidha, alisema uwa katika tamasha
hilo wasanii walipiga miziki ya asili ili kudumisa utamaduni na mila za
mtanzania na kwamba kulingana na idadi kubwa ya watu walioingia zilipatikana
zaidi ya shilingi milioni nane.
Alisema kuwa jumamosi ijayo Saida
Karoli atatumbuiza katika mji wa Bukoba kwenye ukumbi wa Linaz Club na jumapili
atakuwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini humo.
0 comments:
Post a Comment