MBUNGE wa Viti Maalumu, kupitia Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mara, Ester Bulaya, ametoa msaada wa mabati
kwa ajili ya Kituo cha Polisi Bunda na kikundi cha kwaya cha The Disciples of
Christ kilichopata sh milioni moja.
Msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake
aliyoitoa hivi karibuni.
Akikabidhi msaada huo, mwakilishi wa mbunge huyo,
Joash Kunaga, alisema walipewa pesa hizo na mabati na mbunge huyo ambaye kwa
sasa yuko jijini Dar es Salaam kikazi ili waviwasilishe kwa wahusika.
Mlezi wa kwaya hiyo, Beatrice Kuyenga, alimpongeza
Bulaya kwa kutimiza ahadi yake na kwamba pesa walizopata, watazitumia kurekodi
nyimbo mpya za kwaya hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Balili, Ernest Nkonoki,
alisema kitendo alichoonesha mbunge huyo ni cha busara kwani ni viongozi
wachache wanaotimiza ahadi zao kwa wapiga kura.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya
Bunda, ASP Mayunga Raphael, ambaye alipokea mabati hayo yenye thamani ya sh
500,000, alisema yatatumika kwa kazi iliyokusudiwa.
Alisema msaada wa mbunge huyo kwa Polisi unaonesha
namna anavyothamini uwajibikaji wa Jeshi la Polisi wilayani hapo.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment