VIONGOZI na
watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Mara, wametakiwa kuhakikisha wanaelewa pato
la wananchi katika maeneo yao ili kupanga mipango ya maendeleo. Mkuu wa Wilaya
ya Rorya, Elias Goroi, alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha kawaida cha
viongozi na watendaji wa halmashauri za mkoa (ALAT), kinachowaunganisha pamoja
katika kujadili na kuweka mipango ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za
maendeleo, kilichofanyika Septemba 27, wilayani Rorya.
Goroi, aliyefungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa, alisema kujua kiwango cha umaskini cha wananchi kwenye maeneo husika husaidia kuweka mipango yenye tija kwa wananchi.
“Unapoongoza bila kujua kiwango cha umaskini cha wananchi unaowaongoza, unaongoza bila dira,” alisema.
Aliwaasa wajumbe hao kuhakikisha wanasimamia vizuri matumizi ya rasilimali na fedha zinazopelekwa na serikali katika maeneo yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Mara, Joseph Marimbe, ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, akitoa nasaha zake kabla ya kuanza kwa kikao hicho, alisema halmashauri zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuwa tegemezi wa mapato toka serikali kuu, huku zikiwekewa vikwazo zinapobaini vyanzo vya mapato.
Kikao hicho cha ALAT, kilichowashirikisha wenyeviti wa halmashauri, madiwani na wakurugenzi atendaji wa halmashauri zote 7 za Mkoa wa Mara, pamoja na mambo mengine kilijadili jinsi ya kuitumia fursa ya kongamano la uwekezaji kanda ya ziwa, linalotarajiwa kufanyika Novemba, mwaka huu mkoani Mwanza.

Chanzo: Rai
0 comments:
Post a Comment