HALMASHAURI
ya Wilaya ya Tarime imepokea sh.Bilion 8,012,476,466.26 kutoka Mgodi wa
North Mara Barrick kwa ajili ya kuwalipa fidia kwa awamu mbili wananchi waliofanyiwa
uthamini ili kupisha maeneo kwa ajili ya shughuli za mgodi ambapo watu 382
watalipwa,na malipo hayo yatafanyika wakati wowote baada ya kukamilika taratibu
za malipo.
Hayo
yameelezwa mbele ya waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sirari (ccm) Amosi sagara
nakwamba malipo hayo yatalipwa kwa wananchi wa Vitongoji vya Gonsara,
Nyabigena na Nyamichare .
Sagara
amesema kuwa malipo hayo ya fidia yamekuja kufuatia malalamiko ya wananchi
ya muda mrefu ya kuutaka mgodi wa Nyamongo kuwahamisha wananchi waishio jirani
na mgodi ili kuondoa migogoro kadha wa kadha kati ya wananchi na mgodi.
Sagara
ameongeza kuwa kutokana na malalamiko hayo Serikali kupitia Wizara ya ardhi
Nyumba na maendeleo ya makazi ilituma kikosi kazi kushughulikia matatizo
ya uthamini na fidia katika maeneo yanayozunguka mgodi wa North Mara ili
kujenga mahusiano mema kati ya wananchi na Mgodi.
Aidha
Sagara amesema kuwa kati ya fedha hizo sh. Bilion 5,647,225,356.
Zinatarajiwa kulipwa kwa awamu ya 26 na sh.2,365,251,110.26 zinatarajia kulipwa
kwa awamu ya 33 na malipo yatafanyika kwanzia hivi sasa.
Mwenyekiti
ameeleza kuwa halmashauri pia imeweza kuwalipa watu wa kitongoji
cha Nyamichare awamu ya 29 kwa watu 120 jumla ya milioni 477,362,316. Na
watu wote wamelipwa na wamechukua malipo yao.
0 comments:
Post a Comment