MENEJA Forodha wa Mkoa wa
Mara Ben Usaje amesema kuwa Tanzania haitanufaika na jumuia ya Afrika
Mashariki iwapo haitazalisha viwanda ambavyo vingetengeneza bidhaa
kutokana na mali zilizopo na Mataifa yakafika kununua bidhaa hizo
zilizotengenezwa Tanzania ili kuongeza pato la nchi.
Meneja huyo amesema
kuwa Wafanyabiashara wa nchi ya Kenya wamekuwa wakinunua zao la Ufuta na
alizeti kutoka Tanzania na kwenda kutengeneza mafuta katika viwanda vilivyoko
nchini kwao kisha mafuta hayo uyauza Tanzania bila hata kulipa kodi na
wakati mazao yametoka Tanzania.
Usaje ameyasema hayo
hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mbele ya
Waziri wa Afrijka Mashariki Samwel Sita wakati wa Ziara yake Tarime ambapo
waziri huyo aliweza kuzungumza na wananchi juu ya maswala mbalimbali
kuhusiana na soko la jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo Waziri wa
Afrika Mashariki Samweli Sita aliwataka wananchi kutokuwa na mawazo finyu
katika jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo akawashauri wawe na mawazo mapana
kwani kujiunga na jumuiya hiyo kunamanufaa makubwa kwa watanzania ambapo
hatahivyo majibu yake yalidaiwa kuwa ni ya kisiasa.
0 comments:
Post a Comment