Shule 10 za msingi, zimefanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu mkoani Mara.
Shule tisa katika hizo ni za binafsi na moja ya Serikali .
Mkoa wa Mara una jumla ya shule 705 za msingi.
Shule iliyoongoza ni Twibhoki iliyoko wilayani
Serengeti ikifuatiwa na ACT Mara Shule zingine na nafasi zao katika
mabano ni za Olympus (3) Fort Ikoma ambayo ni ya Serikali (4) Bhakita
(5) Day star (6) Enyamahi (7) Imanuel (8) Paroma (9)na Fase
Joma(10).
Akizungumzia matokeo hayo Meneja wa Shule ya
Twibhoki, Grace Nyakwe alisema ushindi wao unatokana na malengo ya jumla
na kujituma kwa walimu.
“Hii ni shule binafsi..wazazi wanaleta watoto hapa
wakiamini kupata elimu bora na ili kufikia matarajio hayo tunaweka
malengo, wanafunzi nao wamekubali kuteseka kwa kusoma,”alisema.
Alisema shule yake, imepania kuendelea kushina
nafasi ya kwanza si tu katika mitihanio, lakini pia kwa kutoa elimu bora
miongoni mwa shule za msingi za Mkoa wa Mara na hata mikoa ya jirani.
CHANZO;MWANANCHI
CHANZO;MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment