.Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya
Bunda, mkoani Mara, wameahidi kushirikiana na wakazi wa wilaya hiyo,
katika kuufanya endelevu, mradi wa chakula cha wanafunzi shuleni hata
baada ya wafadhili kuondoka.
Mradi huo unaoendeshwa katika Wilaya za Bunda na
Butiama za mkoani Mara, umekuwa ukifadhiliwa na Shirika la PCI la
Marekanitangu mwaka 2010 ambalo linatarajia kumaliza shughuli zake mwaka
2016.
Wakizungumza katika warsha maalum iliyoandaliwa na
shirika hilo, madiwani walisema maadam mradi huo umeonyesha mapinduzi
makubwa katika elimu kuna kila sababu ya halmashauri kuuendeleza.
Waliyataja baadhi ya mapinduzi hayo kuwa ni
ongezeko la ufaulu wa wanafunzi, mahudhurio na uandikishaji wa wanaoanza
masomo ya darasa la kwanza.
Madiwani hao walisema watatenga fungu kwenye
bajeti ya halmashauri hiyo kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule
huku wakiitaka jamii kuchangia vyakula.
Walisema hatua hiyo ni ya muhimu katika kuboresha sekta ya elimu katika halmashauri hiyo.
CHANZO;MWANANCHI
CHANZO;MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment