MTU mmoja aliyemtapeli Mkuu wa Mkoa wa Mara na maofisa usalama mkoani
hapa, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu, baada ya kujitambulisha
kuwa yeye ni ofisa usalama kutoka makao makuu mjini Dar es Salaam.
Tapeli huyo, alisema ametumwa kwenda kukagua na kutambua uuzaji wa risasi na bunduki kutoka Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (27KJ Makoko), kilichoko mjini Musoma.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo Juni 17, mwaka huu mtuhumiwa, Liso Chacha alimpigia simu Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa kuwa yeye ni ofisa usalama kutoka makao makuu aliyeagizwa kufuatilia mtandao wa kuuza risasi na bunduki kutoka kikosi cha 27 KJ.
Hakimu Maganga, alidai baada ya RC Tupa kupata taarifa hizo alimpigia simu Mkuu wa Kikosi cha Jeshi cha Makoko, akimtaka kuwasiliana na mtuhumiwa huyo kwa lengo la kufanikisha shughuli aliyotumwa.
Alidai ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wa watu saba wa upande wa mashitaka, ulikuwa ukimtuhumu mshitakiwa kuwa alikuwa akijitambulisha kuwa yeye ni ofisa usalama kuwataka wampe ushirikiano.
Alisema mshtakiwa huyo, alipokelewa na ofisa wa JWTZ, kisha kupewa malazi katika nyumba ya mapumziko, ambapo aligharamiwa chakula na huduma nyingine muhimu.
Alidai siku iliyofuata, uongozi wa JWTZ ulikutana na Ofisa wa Jeshi la Polisi kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kwa lengo la kumsaidia kumpa ulinzi mtuhumiwa huyo ili afanye upekuzi.
Baada ya hapo mtuhumiwa, alipewa askari wa FFU wawili ambao aliambatana nao kwa ajili ya ukaguzi wa magari kwa muda wa siku mbili.
Kwa upande wa Idara ya Usalama wa Taifa makao makuu, walipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo walidai hawajatuma mtu kufanya shughuli ya aina hiyo mkoani.
Mwendesha mashitaka wa polisi, Stephano Mgaya aliiambia Mahakama kuwa mtuhumiwa alifanya kosa la jinai kuidanganya Serikali na kuchafua vyombo vya dola kuwa ni mtumishi wa umma na pia ameagizwa na idara ya Usalama Makao Makuu kufanya uchunguzi wa mtandao wa wizi wa silaa, jambo ambalo ni uongo.
Alisema mtuhumiwa anastahili adhabu kali kwa kuipaka Serikali matope ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia ya kufanya udanganyifu wa kujipa nyadhifa ambazo sio zao na kufanya utapeli.
Chanzo;Mtanzania

0 comments:
Post a Comment