MBUNGE wa Jimbo la
Tarime Nyambari Nyangwine (CCM) ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Tanapa amesema
kuwa elimu ya uhifadhi inapaswa kutolewa zaidi kwa wananchi
wanaoishi jirani na hifedhi ya Taifa ya Serengeti ili wananchi wajue umuhimu na
uchumi unaotokana na hifadhi .
Nyangwine amesema
kuwa Tanapa na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wanapaswa kuwaelimisha wananchi
juu ya mipaka ya hifadhi kwani kutokuwepo kwa elimu ya kutosha juu ya mipaka
iliyowekwa imesababisha wananchi kuzidi kulisha mifugo yao ndani ya hifadhi.
Nyangwine ameyasema
hayo wakati akiwakabidhi waandishi wa habari wa magazeti wa Wilayani Tarime
kamera 7 za kisasa zenye jumla ya thamani ya milioni 1,750000 ili waweze
kuzitumia katika shughuli zao za kihabari Wilayani Humo.
Nyangwine
ameongeza kuwa mipaka ya Bonde la Nyanungu iko kisheria na haliwezi
kurudishwa kwa wananchi kwakuwa bondi hilo liko kwenye hifadhi ambayo ni
kivutio cha mahajabu ya Dunia na kupitia hifadhi hiyo inachangia kuongeza pato
la Nchi.
Nyangwine amesema
kuwa kwa muda mrefu wananchi wanaozungukwa na bonde hilo wamekuwa
wakishinikiza kuachiwa bonde kwa ajili ya shughuli za malisho na
hivyo kujikuta wakiingia migogoro na Tanapa.
0 comments:
Post a Comment