MADIWANI Wilayani Rorya Mkoani
Mara wamegomea kikao cha Kupitisha bajeti ya Halmashauri ya
2014/2015 kwa madai kuwa kikao hakikuzingatia mudana bila hivyo
wasingeweza kujadili bajeti kwa undani na hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri
Charles Ochele Ambaye ni Diwani wa Kata ya Roche kulazimika khairisha kikao
hadi januari 3/2014.
Wakiwa kwenye kikao jana kwenye
ukumbi wa Halmashauri Madiwani wamesema kuwa hawawezi kujadili bajeti
kwakuwa kikao kilianza saa 9 alasiri na wao kama wawakilishi wa wananchi
ni lazima waijadili bajeti hiyo kwa mapana zaidi juu ya yaliyomo kwenye
makablasha .
Aidha madiwani wasema kuwa
hawawezi kujadili bajeti kwa siku mmoja kwani kwakuwa bajeti ni swala nyeti
ilipaswa kujadiliwa kwa muda wa siku mbili kama halmashauri zingine ikiwemo Halmashauri
ya Tarime iliyojadili bajeti kwa muda wa siku Mbili.
Pia Wameongeza kuwa wameshangazwa
baada ya kutakiwa kujadili bajeti bila hata bajeti hiyo kujadiliwa kwenye vikao
vya vyama ili waichambue kujua mapungufu yaliyomo na badala yake
ikawasilishwa moja kwa moja kwenye Baraza la Madiwani bila kujadiliwa kwenye
vyama kwaza.
0 comments:
Post a Comment