UONGOZI wa Serikali
ya kijiji cha Kerende Kata ya Kemambo Wilayani Tarime wameutaka Mgodi wa North
Mara Barrick kutekeleza miradi kwa mujibu wa makubaliano yao na kijiji ya April
14,mwaka 2012 kwa madai kuwa mgodi umekuwa hautekelezi miradi na mingine
kutokukamilishwa kwa wakati.
Mwenywekiti wa jiji
cha Kerende Mambaga Muhamed amesema kuwa kwa mujibu wa makubaliano kijiji
kilitakiwa kutoa watu 30 kwa ajili ya kupewa maeneo ya ulinzi kwenye
Mgodi badala yake nafasi hizo wamepewa taasisi binafsi bila serikali za jijiji
kushirikishwa.
Muhamed amesema kuwa
Mgodi umeshindwa kutekeleza huduma za umeme katika kijiji hicho ambapo maradi
huo ulitakiwa kukamilika Octoba 2013 na haujafanyika,ambapo pia mgodi
umeshindwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa zahanati uliotakiwa kukamilika
Desemba 2013.
Muhamed ameongeza
kuwa Mgodi umeshindwa kukamilisha mradi wa ukarabati na ujenzi wa shule ya
msingi Kerende ambapo bilioni 3.2 zilitolewa na mgodi kwa maswala
ya elimu na hadi sasa Mgodi umetumia milioni 780 kwa ujenzi wa shule ya
Sekondari ya Kemambo huku bado ukiendelea kuwa na vipolo vingi vya ujenzi licha
yakutolewa fedha nyingi na Mgodi.
Hata hivyo Ofisa
mahusiano wa Mgodi wa North Mara Suleman Monata alipotafutwa kwa njia ya simu
kujibu tuhuma hizo zilizotolewa na Uongozi wa Serikari ya kijiji Cha Kerende
simu yake haikupatikana na juhudi za kumtafuta ajibu tuhuma zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment