WAJASILIAMALI WAKIPEWA MAELEZO |
AFISA MFAWIDHI WA PSPF MKOA WA MARA SUDI HAMZA AKIMUHUDUMIA MWANACHAMA KATIKA OFISI ZA MFUKO HUO JENGO LA TTCL MJINI MUSOMA |
Afisa
Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) mkoa wa Mara
Sudi Hamza ametoa wito kwa Wajasiliamali kuweka utaratibu wa kujiwekea
akiba katika mifuko ya
pensheni ili kujipatia mafao ambayo yataweza kuwakomboa kipindi ambacho
mjasiliamali atakuwa amekwama katika jambo lolote.
Akizungumza na blog hii ofisini kwake,Sudi Hamza amesema mfuko wa uchangiaji wa hiari
ulioanzishwa na (PSPF) lengo lake hasa ni kuwawezesha wajasiliamali kujiwekea akiba
baada ya mifuko mingi kuwalenga watumishi wa umma na kada nyingine.
Amesema
wajasiliamali wanapaswa kuangalia faida ya kujiwekea akiba kwani
humkomboa pale atakapokwama ikiwa ni suala la ada ya elimu ama
kujiongezea mitaji katika biashara pale kutakapotokea kukwama na
kuhitaji mafao ya kujikomboa.
Amesema awali mfuko huo ulikuwa ukiwatazama watumishi wa umma pekee yao
katika kujiwekea mafao ya pensheni lakini utaratibu mpya ni fursa nyingine kwa
wajasiliamali pamoja na watu wengine wasio watumishi wa umma katika
kujiwekea akiba.
Akizungumzia
fao la kujitoa ambalo limekuwa likizungumziwa usumbufu wake kwa baadhi
ya mifuko,Sudi amesema PSPF kitu ambacho inakizingatia ni kutomuona
mwanachama wa mfuko huo akiangaika katika kufatilia mafao.
Amesema
utaratibu uliopo wa mwanachama kuandika barua mapema juu ya kutaka
kujitoa ama kuhitaji mafao kwa ajili ya elimu ama ujasilimali unasaidia
kumuandalia mwanachama fao lake kwa muda anaohitaji bila kumletea
usumbufu.
Afisa huyo wa PSPF amesema kwa muda wa siku tatu tangu waanze uhamasishaji wa uchangiaji wa hiari kwenye maonyesho ya SIDO mjini Musoma jumla ya wanachama 26 wameshajiunga na kuwaomba wajasiliamali wa mkoa wa Mara kufika katika ofisi mpya za mfuko huo zilizopo katika jengo la shirika la simu TTCL mjini musoma waweze kujiunga
Afisa huyo wa PSPF amesema kwa muda wa siku tatu tangu waanze uhamasishaji wa uchangiaji wa hiari kwenye maonyesho ya SIDO mjini Musoma jumla ya wanachama 26 wameshajiunga na kuwaomba wajasiliamali wa mkoa wa Mara kufika katika ofisi mpya za mfuko huo zilizopo katika jengo la shirika la simu TTCL mjini musoma waweze kujiunga
0 comments:
Post a Comment