Home » » WANAWAKE TARIME WAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

WANAWAKE TARIME WAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

WANAWAKE  Wilayani Tarime wanaongoza kwakuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi  ukilinganisha na wanaume  ambapo miongoni mwa sababu zinazochangia ni mira  potofu za ndoa za jinsia moja (Nyumba Intobhu),kurithi wajane,ndoa  za wake wengi,ukeketaji,kuachana kwa wanandoa na umasikini wa kipato .

Akisoma Risala Mbele ya Mgeni rasmi Machango Jonathani  katika maadhimisho ya siku ya ukimwi Juma Wilisoni amesema kwa mwaka 2011-2012 wanawake wapatao 251 walikutwa na maambukizi huku wanaume  133 wakiwa na maambukizi ambapo kwa mwaka 2012-2013 wanawake wapatao 170 wakiwa na maambukizi na wanaume 61 wakiwa na maambukizi.


Katibu wa Afya  Hospitali ya Wilaya ya Tarime Sufiani Mageta  amesema kuwa   katika kampeni za kupima kwa hiari kwa kushirikiana na mradiwa Razhed- Africare na Mgodi wa North Mara watu 6355 wamepima kati ya hao wanawake 44 wamekutwa na maambukizi, wanaume wakiwa 24 huku  watumishi  wa Mgodi wa North Mara 30 kati ya 1320 waliopima wamekutwa na maambukizi.

Hata hivyo  Katibu tarafa  ya Inchage Machango Jonathani  aliyekuwa mgeni rasmi  ameitaka jamii  kuachana na mila potofu kwani zinachangia kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi na akawasisitiza waanchi kutowanyanyapaa  waathirika wa ukimwi ili  wazii kujitokeza kupima afya zao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa