Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema),Vicent Nyerere
Silima aliyasema hayo jana wakati akijibu Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere, aliyetaka kujua kama Serikali ina mpango wa kuwanunua nguo wafungwa hao kuwa nusu uchi kutokana na wanazovaa kuchakaa.
Silima alisema wafungwa hao watapewa nguo hizo mpya hivi karibuni.
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Anna Mallac, alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuongeza vyumba vingine katika gereza la Mpanda ili kukabiliana na msongamano wa mahabusu na kukarabati nyumba za askari kutokana na uchakavu wa kutisha.
Silima alisema serikali inatambua matatizo ya ufinyu wa nafasi ya uliopo katika magereza nchini likiwamo la Mpanda.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, serikali kupitia Jeshi la Magereza imekuwa ikitatua tatizo hilo kwa awamu kwa kufanya ukarabati na kupanua magereza ya zamani, kukamilisha magereza ambayo ujenzi wake haujakamilika na kujenga mapya kwenye wilaya zisizokuwa na magereza.
Alisema kwa mujibu wa Mpango wa miaka 15 wa kuboresha hali ya magereza nchini, gereza hilo la Mpanda ni miongoni mwa magereza yatakayofanyiwa ukarabati na upanuzi katika mwaka wa fedha 2014/15.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment