BARAZA la mamlaka ya mji mdogo wa
Bunda, mkoani Mara, jana limemkataa mkaguzi wa barabara wa halmashauri ya
wilaya hiyo, kwa madai kuwa hawajibiki ipasavyo katika kufungua na kulima
barabara katika mji huo.
Mkaguzi wa barabara wa wilaya hiyo, Bw.
Martin Jahulula, amekataliwa na baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, jana
kwenye kikao cha kupitisha bajeji ya mwaka wa fedha wa 2014/2015 kilichofanyika
mji Bunda.
Wakichangia katika kikao hicho
wenyeviti wa vitongoji katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, wamesema kuwa
Jahulula amekuwa hawajibiki ipasavyo katika kutekeleza majukumu yake, hali
ambayo inasababisha mji huo huoa kutokuwa na barabara zenye ubora.
Wamesema kuwa amekuwa akijipangia yeye
mwenyewe barabara anazotaka kulima bila kushirikisha maamuzi ya vikao wala
wenyeviti wa vitongoji husika na kwamba pia amekuwa akifanya hivyo katika
mazingira ya kuomba rushwa.
Hata hivyo hawakufafanua kuwa ni rushwa
ya kiasi gani na kutoka wapi ambayo amekuwa akiiomba au kuichukuwa katika
mazingira hayo.
Aidha wamesema kuwa kutokana na
barabara za mji huo kutokulimwa na kuwa na ubora unaotakiwa, hali hiyo
itasababisha mji huo kutokupandishwa na kuwa mji kamili, kwa sababu kigezo
mojawapo ni kuwa na barabara zenye ubora.
Kufuatia hali hiyo wenyeviti hao
walimtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bw. Simoni Mayeye, kumuondoa
kwenye nafasi hiyo mtalaamu huyo na kumtafutia kazi nyingine na kuongeza kuwa
hawako tayari kufanya naye kazi.
0 comments:
Post a Comment