KIJIJI cha Ikoma robanda kata ya Ikoma wilaya ya Serengeti
Mkoani Mara kimepitisha makadirio ya kukusanya sh.251,601,065.80
kutoka vyanzo vyake vya ndani,ambazo zitasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo
kusomesha wanafunzi na msaada kwa wazee na wasiojiweza.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho Itabe Nkiri ameiambia Rediao Free
Africa kuwa bajeti hiyo ya 2014 imepitishwa na mkutano mkuu wa kijiji na kamati ya Maendeleo ya kata(WDC), kuwa atakusanya fedha kutoka kambi za kitalii, ikiwa ni ushuru wa pango la ardhi na vitanda na maji.
Kuhusu matumizi amesema sekta ya elimu imepewa kipaumbele ambayo imetengewa sh.88,689,065,afya 37,400,000,huduma za jamii 42,272,000,kilimo na mifugo 6,240,000, Maliasili na
utalii,sh.mil.3,Ulinzi na usalama sh.37,500,000 na utawala 35,960,000.
Aidha wanakusudia kumalizia viporo vya miradi ambayo haikukamilika ,ikiwa ni kukamilisha ujenzi wa sekondari ya kijiji,kuchangia wanafunzi wa chuo kikuu 10,kidato cha v-vi 10 ,wanafunzi wa vyuo vya kati na ufundi kwa zaidi ya sh.mil.60.
Nkiri amebainisa kuwa wanalenga kutengeneza madawati kwa
shule ya msingi Robanda,ujenzi wa chuo cha utalii kijijini hapo,kuwahudumia wazee
,vikongwe na wasiojiweza 40 waliopo kijijini hapo kwa kuwanunulia chakula na
blanketi kwa mwaka mzima.
Kijiji hicho ni cha kwanza kwa wilaya hiyo kuwa na mipango
inayotekelezeka kwa kutegemea mapato yao ya ndani,kulipia wanafunzi na kusaidia wazee wasiojiweza.
0 comments:
Post a Comment