ILI kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma za jamii, serikali
ya kijiji cha Makundusi Kata ya Natta wilaya ya Serengeti mkoani Mara,imetumia
zaidi ya sh.mil.51 kwa ajili ya kulipia nishati ya Umeme kwa wakazi na
taasisi zake.
Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hicho Juma Porini amesema kuwa fedha hizo zimetokana na mapato kutoka vyanzo mbalimbali kama malipo ya pango kutoka kampuni ya Grumeti Fund, mapato
kutoka WMA ,ambapo kijiji ni mwanachama.
Amesema kwa kuwa kijiji hakiko kwenye mpango wa umeme vijiji (REA) kwa pamoja wameamua kulipia ili kuharakisha maendeleo kwa jamii ,sambamba na huduma nzuri kwenye taasisi za umma kama shule, zahanati na ofisi ya kijijini.
Porini amesema kuwa kupata umeme hapo kijijini kutafungua fursa ya ajira na kusukuma maendeleo, kwa kuwa wananchi,wataanzisha shughuli za ufundi wa kuchomelea vyuma, kuchaji simu, uuzaji wa soda, maji na mambo mengine yanayohitaji umeme,pia watalazimika kujenga nyumba za kisasa.
Aidha amesema wamefungua mnada mkubwa kijijini hapo unaojumuisha wafanyabiashara kutoka wilaya za mkoa wa Mara na nje ya nje ya mkoa,hivyo kupata umeme kutaharakisha maendeleo kijijini.
Amewataka wananchi kuanza maandalizi pindi Tanesco watakapo kuwa wamemaliza kazi yao ,waweze kunufaika na nishati hiyo muhimu,waweze kuweka umeme kwenye majumba yao.
Hata hivyo imebainika kuwa ukosefu wa vifaa kwa shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)nichanzo cha mradi huo kuchelewa kuanza kutekelezwa.
0 comments:
Post a Comment