MADIWANI
WA Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara wameitaka Serikali
kuingilia kati kitendo cha wananchi kutozwa fedha kwa wagonjwa wao
wanaosafirishwa na gari la wagonjwa(Ambulance) lililotolewa na Serikali
katika Hospitali Teule ya Shirati kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa
kwenda Mikoani kupata huduma za matibabu.
Wakiongea
wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, Diwani wa kata ya Mkoma
ambaye ni mjumbe wa bodi ya Hospitali ya Shirati Kitori Lazaro(Chadema)
amesema kuwa pindi mgonjwa anapougua na kuhitajika kusaforishwa
kwenda hospitali ya Bugando Mkoani Mwanza ndugu utozwa na kuchangia
laki nne na elfu 20 kama posho ya Dereva, Nesi na mafuta
jambo linalowashinda wengi na hivyo wagonjwa kupoteza maisha.
Mganga Mkuu wa Wilaya Gina .E.Gina amesema kuwa kila mwaka Serikali utoa milioni 147 ambazo ni mfuko wapamoja kwenda hospitali ya Shirati nakwamba mwananchi hawapaswi kutozwa fedha yoyote wakati anaposafirishwa mgonjwa akaongeza kuwa huwenda utozwa gaharama kutokana na Serikali kuchelewa kupeleka fedha kwa wakati kwani fedha zilizotakiwa kufika julai zimepokelea Desema 16 mwaka jana.
Diwani
wa kata ya Mirare Piter Ayoyi (ccm) amehimiza Halmashauri kujenga Hospitali ya
Wilaya au kuteuwa kituo cha afya cha serikali kama vile kituo cha
Changuge kilichopo Makao Makuu ya Wilaya ya Rorya kipandishwe hadhi
nakuwa hospitali ya Wilaya na siyo kuendelea kutegemea hospitali teule ya
misheni jambo linalosababisha migongano mikubwa baina ya wananchi na Serikali.
0 comments:
Post a Comment