Home » » ULINZI WAZIDI KUIMARISHWA TARIME

ULINZI WAZIDI KUIMARISHWA TARIME

Jeshi la polisi Mkoa wa Mara  na Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kwa kushirikiana na kikosi cha Oparesheni Kutoka Makao Makuu ya Jeshi la polisi  wanaendelea na zoezi  la kuimarisha usalama na upelelezi dhidi ya jambazi lililouwa watu ambapo usiku wa kuamkia leo hakuna mauwaji yoyote yaliyotokea.

Kutokana na hofu ya waanchi Usuku wa   leo  mida ya jioni wananchi walirejea majumbani kwao na watu kutoonekana wakitembea barabarani ambapo pia askari polisi wakiwa kwenye Difenda za polisi  wamekuwa wakizungukazunguka kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Tarime  wakiwa  na mbwa kwa ajili ya kuimalisha usalama na msako mkali dhidi ya jambazi lisilofahamika ambalo limeuwa watu wapatao saba.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Justus Kamugisha amesema jeshi la polisi limejizatiti vya kutosha kwa kuongeza askari kwa ajili ya msako nakwamba hawezi kusema kuwa kuna usalama wa kutosha nawakati jambazi bado halijakamatwa.

Mkuuwa Wilaya ya Tarime John Henjewele  amesema kuwa ulinzi wa kutosha umeimarishwa na  tangu jumatatu  msako uliongezeka baada ya kutokea mauwaji  na msako umeongezwa kwenye Kata ya Turwa,Kitare,Binagi ambako matukio ya mauwaji yametokea na akawataka wananchi kutoa taarifa za siri pindi wanapopata dalili za mtu wasiye mjua anaingia kwenye maeneo yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa