Home » » WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU SERENGETI KWENDA SEKONDARI

WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU SERENGETI KWENDA SEKONDARI

WANAFUNZI 2,189  kati ya 4,964 waliofanya mtihani  wamechaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari wilayani Serengeti mkoa wa Mara, ufaulu huo ukiwa ni asilimia 44 ikilinganisha na asilimia 24.8 mwaka 2012.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Bi,Goody Pamba amesema,wavulana  waliochaguliwa ni 1,244 na wasichana
945,miongoni mwao wanafunzi 28 wamekwenda bweni wasichana wakiwa 9,wavulana 19.

Amesema  wilaya haina upungufu wa vyumba vya madarasa,hivyo wote waliochaguliwa watakwenda shule ,na kuwasisitiza wazazi, viongozi mbalimbali kuhakikisha wale waliochaguliwa wanaanza masomo.

Mkurugenzi huyo amesema wilaya hiyo imekuwa ya 3 kimkoa ,ufaulu ambao anadai hamridhishi,na kuwa wakaguzi wote wamelipwa posho zao na wanaungana na timu ya wataalam kufuatilia mwenendo wa ufundishaji.

Hata hivyo ufaulu huo ni chini ya Malengo ya Mpango wa Matokeo Makubwa sasa(BRN)ambao unataka ufaulu kuwa asilimia 60.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa