Home »
» Washtakiwa watano jela miaka 90
Washtakiwa watano jela miaka 90
Mahakama
ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, imewahukumu watu watano kati ya saba
kifungo cha miaka 90 kila mmoja baada ya kukutwa na hatia katika makosa
matatu.
Kati ya makosa hayo,
mawili ya ubakaji na moja la unyang'anyi wa kutumia silaha ambapo
washtakiwa wawili, waliachiwa huru baaada ya mahakama kushindwa kuwatia
hatiani.
Hukumu hiyo imetolewa
Desemba 30,2013 ambapo Hakimu Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Bw. Richard
Maganga, aliwataja washtakiwa waliotiwa hatiani kuwa ni Juma Patick
(25), Mirumbe Mwita (28), pamoja na Babu Zacharia (20).
Wengine ni Sokolo
Songoye (21), Deus Butiku (20) ambapo Mirunde Johanes (28) na Msai Elius
Mwita (20) wakiachiwa huru ambapo washtakiwa wote ni wakulima na wakazi
wa
Manispaa ya Musoma, mkoani humo.
"Hawa washtakiwa
walifanya makosa hayo usiku wa Mei 4,2013, katika eneo la Bweri,
Manispaa ya Musoma, kila kosa wamepewa adhabu ya kukaa gerezani miaka
30.
Alisema washtakiwa hao walimbaka msichana mwenye umri wa
miaka 33 (jina tunalo), kila mmoja kwa nyakati tofauti na baada ya
kufanya unyama huo walimbaka msichana wake wa kazi
mwenye umri wa miaka 20 (jina tunalo) kwa zamu.
"Daktari alithibitisha
kuwa wasichana hawa walibakwa baada ya kuwapima na kukuta mbegu za
wanaume zaidi ya mmoja lakini hawakukutwa na maambukizi yoyote,"
alisema.
Katika utetezi wao,
washtakiwa hao walikana kuhusika na tukio hilo lakini baada ya Mahakama
kusikiliza hoja za pande zote hasa ushahidi wa upande wa mashtaka,
irijiridhisha kuwa washtakiwa walihusika na tukio hilo na kutoa adhabu
hiyo.
Pamoja na adhabu hiyo, Mahakama hiyo pia imewaamuru
washtakiwa hao wamlipe fidia msichana waliyembaka awali mwenye miaka 33
sh. milioni mbili kutokana na upotevu wa vitu vyake na ubakaji
walioufanya kama fidia.
Vitu vinavyodaiwa kuibwa na washtakiwa
ni fedha taslimu sh.100,000, televisheni moja aina ya Panasonic yenye
thamani ya sh. 20,000 na radio aina ya Panasonic (180,000).
Vingine ni DVD moja aina ya Samsang (85,000), saa ya mkononi (22000) na simu tatu za mkononi (240,000).
Mwendesha mashitaka
aliyefahamika kwa jina moja la Stephano,alisema upande wa mashtaka
ulikuwa na mashahidi sita akiwemo mlalamikaji pamoja na daktari
aliyemchukua vipimo
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment