Home » » ALIMA BANGI KWENYE ENEO LA SHULE

ALIMA BANGI KWENYE ENEO LA SHULE

WAKAZI  wa kijiji cha Rung'abure kata ya Rung'abure wilayani Serengeti Mkoa wa Mara wametoa mwezi mmoja kwa  mkazi wa kijijini hapo aliyekutwa anaishi eneo la shule na kuendesha kilimo ikiwemo bangi, kuhama kwa hiari,vinginevyo watamhamisha kwa nguvu.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya shule Chacha Joseph Meng'anyi ,amesema wananchi wamefikia hatua hiyo  baada ya uongozi wa serikali ya  kijiji kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Mwita Chacha (Sinabi)ambaye mbali na kuvamia eneo hilo, amekuwa akikata miti ya shule,kuwatishia maisha
walimu ,na kuanzisha kilimo cha bangi.


Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Charles Kibure amesema kutokana na mtuhumiwa kukaidi  maagizo ya serikali  , wananchi wamekutana eneo la tukio  kwa lengo la kumhamisha kwa nguvu ndipo wamekuta amelima bangi eneo la shule na kukabidhiwa ofisa mtendaji wa kijiji kwa hatua za kisheria.


Hata hivyo Mratibu elimu kata hiyo Phinias Ibrahimu amesema, licha ya wananchi kumkamata mtuhumiwa na bangi mtendaji wa kijiji hicho amempeleka mtuhumiwa kituo cha polisi Kenyana bila kielelezo, hali ambayo inazidi kuibua hasira kwa wananchi.


Kaimu ofisa mtendaji William Mkeba amekiri kumpeleka mtuhumiwa polisi bila bangi aliyokutwa nayo shambani kwa madai kuwa ameombwa na baadhi ya wananchi ili mtuhumiwa asije akafungwa.



Polisi wilayani hapa wameahidi kufuatilia na kuwa hawatasita kuchukua hatua dhidi ya watakaobainika kutaka kumkingia kifua mharifu huyo.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa